Kila wakati imesemwa usijaji kitabu kwa muonekano wa picha
yake lakini jina la album mpya ya Mariah Carey ni sawa ukajaji kwa cover yake
ya nyuma. Kama alivyoahidi wiki iliyopita pop diva mwenye umri wa miaka 44
ametaja jina la albamu yake mpya na mchoro wa kibunifu wa kitoto na
kulist majina ya nyimbo zinazopatikana ndani ya albam hiyo ikiwa ni albam
yake ya 14, mchoro huo kweli unamaanisha kitu.Mashabiki wamekuwa wakiongea mambo
mengi wengine wakisema muonekano na jina la albamu eti ni kwamba sasa Mariah Carey
ameamua kuonyesha undani wake zaidi. Kwa nyuma ya cover inaonyesha mchoro wa
kitoto na muandiko wa kitoto inamfanya mtu ajiulize kuwa amewaachia watoto wake
wachague maadhui ya albam yake.Mariah Carey aliiambia Billboard kwamba
ataongelea vitu vingi alivyovipitia maishani mwake katika albam hiyo mpya.. Angali hiyo video hapo
chini Mariah Carey akielezea kuhusu jina la albam yake mpya ya Me, I am Mariah.
No comments:
Post a Comment