Maria akiwa kwenye shamba lake la viazi. |
Maria alikuwa akilala kwenye gunia sakafuni na watoto wake, alikuja kukutana na Mwanaidi mkulima aliyepitia mafunzo ya kilimo, alipata elimu jinsi ya ukulima wa viazi vitamu bora na kupewa mbegu zake. Alifundishwa mbinu mbalimbali za kilimo cha kisasa, mbinu ambazo Maria hakuwa na ujuzi nao.
Vilevile alipata kufundishwa jinsi ya kuuza mazao yake. Wateja walikuwa wakimuuliza siri ya ubora wa viazi vyake kuwa na rangi tofauti, kila mara alikuwa akiwaujibu kuwa uwingi wa vitamini A ndo sababu ya viazi kuwa na rangi ya orenji, vitamini A huongeza kinga kwenye mwili wa binadamu. Kwa kupata mbinu ya biashara aliweza kupata wateja wengi katika biashara yake ya viazi.
Maria akimuonyesha mteja wake ubora wa kiazi |
Maria amepiga hatua kubwa kwa kuuza mbegu bora za viazi, chipsi, biskuti, maandazi, keki na unga vyote kutokana na viazi vitamu.Anafanya kazi kwa juhudi na furaha akijua utafika muda ataondokana na hali duni ya kimaisha kutokana na kilimo chake cha viazi vitamu. Kwa sasa ni kiongozi kwenye kikundi chao cha wakulima na anawafundisha wakulima wenzake alichojifunza kuhusu kilimo cha viazi.
Utengenezaji wa chipsi za viazi. |
Kila anapolala Maria huwa anafikiria kuhusu viazi vitamu, pia ana ndoto za kumalizia ujenzi wa nyumba yake anayoijenga kwa matofali ya kuchoma, kuishi katika sehemu bora, kuinua kiwango cha maisha kwa familia yake na kuwapeleka watoto na wajukuu wake wote shule.
Maria akiangalia hatua ya ujenzi wa nyumba yake aliyofikia. |
No comments:
Post a Comment