Serikali imetoa wito kwa wazazi wa watoto 409
waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2013/2014 na kushindwa kuripoti
katika shule walizopangiwa, waripoti haraka vinginevyo watafikishwa
mahakamani.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo
DEODATUS KINAWIRO, Katibu Tawala wa Wilaya ya Chunya SOSTENETH MAYOKA amewataka
madiwani kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji,kata na wazazi, kuhakikisha
watoto hao wanaripoti katika shule walizopangiwa kwa hiari yao kabla mkono wa
dola haujawafikia.
Afisa elimu Wilaya ya Chunya, CHARLES MWAKALILA
amesema tayari hatua zimeshaanza kuchukuliwa na wanafunzi 186 kati ya 409
wamesharipoti shuleni.
Hata hivyo katika hatua ya kushangaza Diwani wa
Kata ya Mkwajuni CHESCO NGAIRO amekanusha idadi hiyo huku Diwani wa Kata
ya Ngwala DONALD MAGANGA akisema ameanza kufuatilia katika Kata yake.
No comments:
Post a Comment