Mmiliki wa timu ya basketball ya Los
angeles Clippers aliyejivunjia heshima yake kote duniani kwa kuonyesha ubaguzi
Donald Sterling amevunja ukimya nakusema bora angemlipa rafiki wake wa kike V.
Stiviano ili asitoe yale maongezi aliyeongea akiwa nae ambayo yalionyesha
ubaguzi kwa wachezaji wa Los Angeles Clippers “I wish I had just paid her off”,
Donlad Sterlin ameliambia gazeti la Dujour. Sterling alimwambia mwanzilishi wa
gazeti hilo la Dujour Jason Binn kwamba amekuwa akijuzuia kufanya mahojiano na
Barbara Walters na NBA wenyewe. Sauti ya Sterling akitoa maoni ya kibaguzi yalitoka
Jumamosi iliyopita toka amekuwa kimya na watu wengi duniani hawakuwa kimya
ikimjumuisha Kamishna wa NBA Adam Silver ambae Jumanne alimpiga faini ya dola
milioni 2 .5 na kutaka wenzake wanaomiliki timu hiyo kuiuza timu hiyo na
kumtaka Sterling asijiusishe na biashara ya ligi hiyo maisha yake yote
kivyovyote vile.
No comments:
Post a Comment