Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ghalib Bilal akiwasha mwenge wa uhuru wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi Mkoani kagera. |
Mbio za Mwenge wa Uhuru
zimezinduliwa rasmi kitaifa mkoani Kagera..
Akizindua mbio hizo, makamu wa
rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MOHAMED GHARIB BILAL, ameuwasha
mwenge huo na kuukabidhi rasmi kwa kiongozi wa mbio hizo kitaifa RACHEL
KAIBANDA, kabla haujakabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa KAGERA, Kanali Mstaafu
FABIAN MASSAWE, ili uanze mbio zake katika mkoa huo.
Awali akizungumza kabla ya uzinduzi
wa mbio hizo za mwenge, makamu wa rais DK. MOHAMED GHARIB BILAL, amewahimiza
wananchi nchini kote kuzingatia suala la amani, ili waweze kudumisha muungano
utakaoendelea kuwaenzi waasisi wa muungano huo.
Mwenge wa uhuru mkoani Kagera,
utatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi
bilioni kumi na tano.
No comments:
Post a Comment