BALE |
Goli hilo lilidumu hadi dakika ya 90 pale Ramos alipowainua
mashabiki wa Real Madrid kwa kusawazisha na kupelekea kuongezwa dakika nyingine
30. Katika dakika 15 za mwanzo dakika ya 110 Bale alifunga goli la pili, katika
dakika 15 za kipindi cha pili wa muda wa nyongeza dakika ya 18 Marcelo
akaipatia Real Madrid bao na kuvunja kabia matumaini kwa timu ya Atletico
Madrid.
Ronaldo akafungwa kwa mkwaju wa penati dakika ya 120 na kuifanya Real
Madrid kuwa mabingwa wa Uefa 2014 ikiwa ni mara ya 10 na ikiongoza kulichukua
kombe hilo mara nyingi kuliko timu yeyote ya barani Ulaya. Ronaldo anaongoza
kwa kufunga magoli mengi msimu huu kwa idadi ya magoli 17, akifuatiwa na
Ibrahimovic wa PSG ana magoli 10, Diego Costa wa Atletico Madrid na idadi ya
magoli 8, akifuatiwa na Messi nae anamagoli 8 wakiwa wamelingana, Aguero wa Man
City anayo magoli 6.
No comments:
Post a Comment