Wednesday, June 18, 2014

KFC Yachangia Dola 30,000 Za Matibabu Ya Victoria Baada Ya Kumnyanyapaa

KFC ni moja ya migahawa mikubwa sana duniani, KFC imesema itachangia dola 30,000 kwa ajili ya matibabu ya mtoto mwenye miaka 3 ambae aliombwa atoke nje ya mgahawa huo kutokana na jeraha alilokuwa nalo kuwa linawaogopesha wateja.

Pesa hiyo iliyotolewa na Mgahawa huo kwa ajili ya matibabu ya mtoto Victoria, kuanzia hapo ukanza ukurasa ambao ulichangiwa hadi kufikia dola 80,000 ambazo zitatumika katika matibabu.

Mtoto huyo anaitwa Victoria Wilcher alijeruhuwa vibaya mwezi Aprili na mbwa, Bibi yake Kelly Mullins alisema kwamba walikuwa wakielekea nyumbani wakitokea hospitali akasema ampitishe mjukuu wake katika mgahawa huo kwa ajili ya kula viazi vya kusaga (mash potatoes)  ndipo mjukuu wake alipoambiwa aondoke anawaogopesha wateja. 

“Walituambia, “tumeombwa tuwaambie muondoke kwa sababu uso wake unawaogopesha wateja wetu’" Mullins aliiambia WAPT-TV “Victoria alielewa kila kitu walichokisema"
Jambo hilo lilimuacha Victoria na machozi, Victoria alishambuliwa na mbwa na imemuweka sana bibi yake katika hali ngumu. "Upande wake wa kulia wa uso wake umepooza, pia kuna upasuaji anatakiwa afanyiwe, hatajiangalia hata kwenye kioo tena, tulipofika KFC hakuwa anataka kutoka nje ya gari, ana miaka mitatu tu lakin amenyanyapaliwa jinsi alivyo."

 “Haijalishi mtu yukoje, utofauti wake na wengine kama mtu anaogopesha au ana rangi tofauti au chochote kile hatakiwi kutengwa, inanifanya niwe na hasira kwa sababu najua maisha yake yote itakuwa hivi” aliendelea kusema bibi yake Mullins. 

." Msemaji wa KFC alitoa maandishi kwa Associate Press ambayo ilisema kuwa "Kwa haraka tulipojulishwa kuwepo kwa ripoti hii Ijumaa, haraka tumeanza uchunguzi kwa jambo hili la kusikitisha, na halitovumiliwa na KFC, labda iwe vingine kutokana na uchunguzu tunaoufanya, tumeomba msamaha kwa familia ya Victoria na tumeamua kuwasaidia. Kampuni inatoa mchango wa dola 30 kumsaidia katika matibabu yake, Kampuni yote ya KFC ipo nyuma ya Victoria,"n ilisema Kampuni ya KFC.

Babu yake Donald Mullins aliwaua mbwa wawili waliofanya hinyo lakini mumwe wa Kelly  Mullins ambae ni babu wa Victoriampenzi wake mpya baadae  walikamatwa  kwa kosa la kuhatarisha maisha ya Victoria.

Idadi Ya Watumiaji Na Waathirika Wa Dawa Za Kulevya Inatajwa Kuendelea Kuongezeka

Idadi ya Watumiaji na waathirika wa Dawa za kulevya inatajwa kuendelea kuongezeka nchini huku kukiwa na mshituko mkubwa kutokana na matumizi ya dawa hizo kupenya kwa kasi hadi maeneo ya Vijijini.
Hali ni mbaya zaidi kwa Jiji la Dar es salaam ambapo katika kipindi cha mwezi Mei mwaka huu Watumiaji wa Heroin wanaopata tiba ya methadone katika Hospitali za Jiji la Dar es salaam wamefikia 1,526.
Matumizi ya Dawa hizo yanaelezwa  kuwa na madhara mengi kiafya na kijamii ikiwemo kudhoofisha afya za Watumiaji na kuathiri uwezo wao wa kufanya kazi  pamoja na kukumbwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya akili, homa ya ini, moyo mapafu na kifua kikuu.
Hali hiyo inawagusa Viongozi wa Dini ambao wanaamua kukutana na kujadili juu ya namna ya kukabiliana na tatizo hilo kutokana na nafasi waliyonayo katika jamii.
Wakati Viongozi hao waandamizi wa Dini wakieleza hayo baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wanaeleza kusikitishwa na ongezeko la Watumiaji na waathirika wa Dawa za Kulevya nchini akiwemo Mchungaji CHRISTOPHER KALATE wa KKKT Dayosisi ya Pwani na Sheikh ASIF MUYENGA kutoka Taasisi ya Daarul Muhibi.
Kwa Jiji la Dar es salaam hali inaelezwa  kuwa mbaya zaidi kwa Manispaa ya Ilala.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, RAYMOND MUSHI amekiri kuwepo kwa tatizo hilo katika Wilaya yake na kubainisha Mikakati iliyowekwa  kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Kiwango kikubwa cha Dawa za Kulevya zinazoingizwa nchini kupitia Barabara, Bandari na Viwanja vya Ndege zinaletwa kutoka nchi za nje.
Katika Kipindi cha Mwezi Januari, mwaka 2013 hadi Mwezi Mei, mwaka huu Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kimefanikiwa kukamata zaidi ya kilo 98 elfu za dawa za kulevya .

Zaidi Ya Wakazi 200 Wa Manispaa Ya Musoma Wanatarajia Kunufaika Na Mradi Mpya Wa Maji

Zaidi ya wakazi laki mbili wa Manispaa ya musoma wanatarajia kunufaika na mradi mpya wa maji unaotarajiwa kukamilika December mwaka huu.
mhandisi wa mradi huo JAILOS CHILEWA amebainisha hayo wakati akitoa maelezo kwa viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi ccm katika ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo uliotarajiwa kukamilika mwezi june mwaka huu ambao utagharimu shilingi bilioni 41.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi musoma mjini DAUDI MISANGO amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua utetekelaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ili kufahamu maendeleo ya mradi huo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Musoma JACKSON MSOME amesema mradi huo ukikamilika unakusudia kumaliza matatizo ya upungufu wa maji kwa  zaidi ya silimia 95 kwa wakazi wa musoma na vitongoji vya jirani.

Polisi Kenya Wamesema Kuwa Wamewakamata Washukiwa Wawili Wa Mashambulizi

Polisi nchini Kenya wamesema kuwa wamewakamata washukiwa wawili wa mashambulizi yaliyofanyika mjini Mpeketoni, Pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 60.
Kundi la wapiganaji wa Al Shabaab limekiri kufanya mashambulizi hayo yaliyofanyika Jumapili usiku na Jumatatu usiku ingawa serikali ya Kenya imesema kuwa mashambulizi hayo yalichochewa kisiasa.
Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba yake kwa taifa, amelaumu vikundi vya wanasiasa pamoja na makundi ya watu ambayo yana nia ya kufaidi kutokana na hali mbaya ya usalama nchini humo kwa kufanya mashambulizi hayo.
Maafisa kadhaa wa polisi wa eneo la Mpeketoni, wamefukuzwa kazi na wengine kuhamishwa kutoka vituo vyao vya kazi katika eneo hilo.
Hii ni baada ya tuhuma dhidi yao kuwa walipuuza onyo la kutokea kwa mashambulizi hayo kutoka kwa shirika la ujasusi na Wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka.

Wednesday, June 4, 2014

Mmiliki Wa Nyimbo Za Bob Marley Aamuliwa

Bob Marley
Mzozo wa kisheria juu ya nani anayemiliki baadhi ya nyimbo maarufu za reggae duniani umemalizika mjini London.
Nyimbo hizo zilizotungwa na kuimbwa na msanii Bob Marley zimekuwa ziking'ang'aniwa na kampuni 2 pinzani juu ya umiliki wao.
Jaji katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata umaarufu 'No Woman, No Cry' kuwa haina haki nazo tena.

Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992.
Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo.
Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.
(By BBC).

Marehemu George Tyson Aagwa Viwanja Vya Leaders Club Jijini Dar es salaam

Mwili wa marehemu George Tyson ukiwasili katika viwanja vya Leaders club jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuagwa, alifariki siku ya Ijumaa 30 Mei 2013 kwa ajali ya gari akitokea Dodoma na anategemea kuzikwa Jumamosi 14 Juni 2014 nchini Kenya.
Wasanii wa Bongo Movies wakiwa wamebeba jeneza la marehemu George Tyson siku ya Jumatano 5 Juni 2014 katika viwanja vya Leaders club jijini Dar es salaam, George Tyson atazikwa tarehe 14 Juni 2014 nchini Kenya.
 
Meya wa Ilala Jerry Slaa akiaga mwili wa marehemu Geroge Tyson.
Sonia mtoto wa marehemu na Monalisa aliyekuwa mke wa marehemu Monalisa (kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Meck Sadick akizungumza kwenye msiba wa marehemu George Tyson 
 Mboni Masimba
 Wasanii wa filamu Tanzania
 Mchungaji akiongoza misa
Waombolezaji
 Wafanyakazi wa TV 1 alipokuwa akifanya kazi marehemu mara ya mwisho kabla ya umauti wakiaga
.Mboni Masimba Mtangazaji wa The Mboni Show akiwasili katika viwanja vya Leaders club kwa ajili kuaga mwili wa marehemu George Tyson
 Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akiaga mwili wa marehemu George Tyson.

Sunday, June 1, 2014

Mwanamke Aliyebadili Dini Apata Utetezi

Afisa mmoja mwandamizi katika wizara ya maswala ya kigeni nchini Sudan amesema kuwa mwanamke aliyepewa hukumu ya kifo kwa kubadili dini yake ya kiislamu,Meriam Ibrahim atawachiliwa huru katika kipindi cha siku chache zijazo.
Abdullahi Alzareg ambaye ni katibu katika wizara hiyo amesema kuwa Sudan inatilia maanani uhuru wa kuabudu na kwamba serikali itamtetea mwananmke huyo.

Kumekuwa na shutma za kimataifa kuhusu hukumu aliyopewa mwanamke huyo.
Meriam Ibrahim anazuiliwa katika jela moja ambapo alijifungua mtoto wa kike juma hili.
Ameolewa na mkristo na pia amehukumiwa kuchapwa viboko mia moja kwa kuzini kwa sababu mwanamke wa kiislamu kuolewa na mkristo ni haramu kulingana na sheria za Sudan.
(By BBC)