Polisi nchini Uturuki wamefyatua mabomu ya kutoa machozi
jana Jumamosi(31.05.2014)wakiwatawanya waandamanaji katikati ya mji wa Istanbul
wakati wa kumbukumbu ya mwaka mmoja ya maandamano makubwa kuipinga serikali.
Polisi walijiweka katika mstari mrefu kuwazuwia wanaharakati ambao walitarajia kusoma taarifa yao katika uwanja wa Taksim na kuweka maua katika uwanja huo katika kumbukumbu ya vifo vya kiasi watu sita katika maandamano dhidi ya utawala wa waziri mkuu Tayyip Erdogan.
Watu wengine sita wameuwawa katika machafuko yaliyotokea bila kutarajiwa katika miezi iliyofuatia wakati hasira dhidi ya Erdogan na chama chake cha AK zikitokota.
Maandamano ya mitaani huenda ni kitu kitakachojitokeza mara kwa mara katika wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa rais hapo Agosti ambapo Erdogan anatarajiwa kugombea, lakini wachache wanatarajia hali hiyo kuzusha athari kubwa za kisiasa kwa kiongozi huyo ambaye ameshika wadhifa wa waziri mkuu mara tatu.
Afisa wa ngazi ya juu wa chama cha AK amesema siku ya Jumamosi kuwa Erdogan atagombea wadhifa wa urais na kuiongoza Uturuki hadi 2023.
Karibu na uwanja wa Taksim, mamia ya watu waliimba , "jiuzulu, wauwaji AKP" na "kila mahali ni Taksim, kila mahali ni upinzani" kabla ya polisi kufyatua gesi ya kutoa machozi dhidi ya kundi la watu, na kuwalazimisha kurudi nyuma
No comments:
Post a Comment