KFC ni moja ya migahawa mikubwa sana duniani,
KFC imesema itachangia dola 30,000 kwa ajili ya matibabu ya mtoto mwenye miaka
3 ambae aliombwa atoke nje ya mgahawa huo kutokana na jeraha alilokuwa nalo
kuwa linawaogopesha wateja.
Pesa hiyo iliyotolewa na Mgahawa huo kwa
ajili ya matibabu ya mtoto Victoria, kuanzia hapo ukanza ukurasa ambao
ulichangiwa hadi kufikia dola 80,000 ambazo zitatumika katika matibabu.
Mtoto huyo anaitwa Victoria Wilcher
alijeruhuwa vibaya mwezi Aprili na mbwa, Bibi yake Kelly Mullins alisema kwamba
walikuwa wakielekea nyumbani wakitokea hospitali akasema ampitishe mjukuu wake katika
mgahawa huo kwa ajili ya kula viazi vya kusaga (mash potatoes) ndipo mjukuu wake alipoambiwa aondoke
anawaogopesha wateja.
“Walituambia, “tumeombwa tuwaambie muondoke
kwa sababu uso wake unawaogopesha wateja wetu’" Mullins aliiambia WAPT-TV
“Victoria alielewa kila kitu walichokisema"
Jambo hilo lilimuacha Victoria na machozi,
Victoria alishambuliwa na mbwa na imemuweka sana bibi yake katika hali ngumu.
"Upande wake wa kulia wa uso wake umepooza, pia kuna upasuaji anatakiwa
afanyiwe, hatajiangalia hata kwenye kioo tena, tulipofika KFC hakuwa anataka
kutoka nje ya gari, ana miaka mitatu tu lakin amenyanyapaliwa jinsi
alivyo."
“Haijalishi
mtu yukoje, utofauti wake na wengine kama mtu anaogopesha au ana rangi tofauti
au chochote kile hatakiwi kutengwa, inanifanya niwe na hasira kwa sababu najua
maisha yake yote itakuwa hivi” aliendelea kusema bibi yake Mullins.
." Msemaji wa KFC alitoa maandishi kwa
Associate Press ambayo ilisema kuwa "Kwa haraka tulipojulishwa kuwepo kwa
ripoti hii Ijumaa, haraka tumeanza uchunguzi kwa jambo hili la kusikitisha, na
halitovumiliwa na KFC, labda iwe vingine kutokana na uchunguzu tunaoufanya,
tumeomba msamaha kwa familia ya Victoria na tumeamua kuwasaidia. Kampuni inatoa
mchango wa dola 30 kumsaidia katika matibabu yake, Kampuni yote ya KFC ipo
nyuma ya Victoria,"n ilisema Kampuni ya KFC.
Babu yake Donald Mullins aliwaua mbwa wawili
waliofanya hinyo lakini mumwe wa Kelly
Mullins ambae ni babu wa Victoriampenzi wake mpya baadae walikamatwa
kwa kosa la kuhatarisha maisha ya Victoria.
Wednesday, June 18, 2014
Idadi Ya Watumiaji Na Waathirika Wa Dawa Za Kulevya Inatajwa Kuendelea Kuongezeka
Idadi ya
Watumiaji na waathirika wa Dawa za kulevya inatajwa kuendelea kuongezeka nchini
huku kukiwa na mshituko mkubwa kutokana na matumizi ya dawa hizo kupenya kwa kasi
hadi maeneo ya Vijijini.
Hali ni
mbaya zaidi kwa Jiji la Dar es salaam ambapo katika kipindi cha mwezi Mei mwaka
huu Watumiaji wa Heroin wanaopata tiba ya methadone katika Hospitali za Jiji la
Dar es salaam wamefikia 1,526.
Matumizi ya
Dawa hizo yanaelezwa kuwa na madhara mengi kiafya na kijamii ikiwemo
kudhoofisha afya za Watumiaji na kuathiri uwezo wao wa kufanya kazi
pamoja na kukumbwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya akili, homa ya ini, moyo
mapafu na kifua kikuu.
Hali hiyo
inawagusa Viongozi wa Dini ambao wanaamua kukutana na kujadili juu ya namna ya
kukabiliana na tatizo hilo kutokana na nafasi waliyonayo katika jamii.
Wakati Viongozi
hao waandamizi wa Dini wakieleza hayo baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo
wanaeleza kusikitishwa na ongezeko la Watumiaji na waathirika wa Dawa za
Kulevya nchini akiwemo Mchungaji CHRISTOPHER KALATE wa KKKT Dayosisi ya Pwani
na Sheikh ASIF MUYENGA kutoka Taasisi ya Daarul Muhibi.
Kwa Jiji la Dar
es salaam hali inaelezwa kuwa mbaya zaidi kwa Manispaa ya Ilala.
Kaimu Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, RAYMOND MUSHI
amekiri kuwepo kwa tatizo hilo katika Wilaya yake na kubainisha Mikakati
iliyowekwa kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Kiwango kikubwa
cha Dawa za Kulevya zinazoingizwa nchini kupitia Barabara, Bandari na Viwanja
vya Ndege zinaletwa kutoka nchi za nje.
Katika Kipindi cha Mwezi Januari, mwaka 2013 hadi
Mwezi Mei, mwaka huu Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchini
kimefanikiwa kukamata zaidi ya kilo 98 elfu za dawa za kulevya .
Zaidi Ya Wakazi 200 Wa Manispaa Ya Musoma Wanatarajia Kunufaika Na Mradi Mpya Wa Maji
Zaidi ya wakazi
laki mbili wa Manispaa ya musoma wanatarajia kunufaika na mradi mpya wa maji
unaotarajiwa kukamilika December mwaka huu.
mhandisi wa
mradi huo JAILOS CHILEWA amebainisha hayo wakati akitoa maelezo kwa viongozi na
wanachama wa chama cha mapinduzi ccm katika ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya
mradi huo uliotarajiwa kukamilika mwezi june mwaka huu ambao utagharimu
shilingi bilioni 41.
Mwenyekiti wa
chama cha mapinduzi musoma mjini DAUDI MISANGO amesema lengo la ziara hiyo ni
kukagua utetekelaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ili kufahamu maendeleo ya
mradi huo.
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya Musoma JACKSON MSOME amesema mradi huo ukikamilika unakusudia
kumaliza matatizo ya upungufu wa maji kwa zaidi ya silimia 95 kwa wakazi
wa musoma na vitongoji vya jirani.
Polisi Kenya Wamesema Kuwa Wamewakamata Washukiwa Wawili Wa Mashambulizi
Polisi nchini
Kenya wamesema kuwa wamewakamata washukiwa wawili wa mashambulizi yaliyofanyika
mjini Mpeketoni, Pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 60.
Kundi la
wapiganaji wa Al Shabaab limekiri kufanya mashambulizi hayo yaliyofanyika
Jumapili usiku na Jumatatu usiku ingawa serikali ya Kenya imesema kuwa
mashambulizi hayo yalichochewa kisiasa.
Rais Uhuru
Kenyatta katika hotuba yake kwa taifa, amelaumu vikundi vya wanasiasa pamoja na
makundi ya watu ambayo yana nia ya kufaidi kutokana na hali mbaya ya usalama
nchini humo kwa kufanya mashambulizi hayo.
Maafisa
kadhaa wa polisi wa eneo la Mpeketoni, wamefukuzwa kazi na wengine kuhamishwa
kutoka vituo vyao vya kazi katika eneo hilo.
Hii ni
baada ya tuhuma dhidi yao kuwa walipuuza onyo la kutokea kwa mashambulizi hayo
kutoka kwa shirika la ujasusi na Wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu
mashitaka.
Wednesday, June 4, 2014
Mmiliki Wa Nyimbo Za Bob Marley Aamuliwa
Bob Marley |
Jaji katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata umaarufu 'No Woman, No Cry' kuwa haina haki nazo tena.
Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992.
Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo.
Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.
(By BBC).
Marehemu George Tyson Aagwa Viwanja Vya Leaders Club Jijini Dar es salaam
Mwili wa marehemu George Tyson ukiwasili katika viwanja vya Leaders club
jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuagwa, alifariki siku ya Ijumaa 30
Mei 2013 kwa ajali ya gari akitokea Dodoma na anategemea kuzikwa
Jumamosi 14 Juni 2014 nchini Kenya.
Wasanii wa Bongo Movies wakiwa wamebeba jeneza la marehemu George Tyson
siku ya Jumatano 5 Juni 2014 katika viwanja vya Leaders club jijini Dar
es salaam, George Tyson atazikwa tarehe 14 Juni 2014 nchini Kenya.
Meya wa Ilala Jerry Slaa akiaga mwili wa marehemu Geroge Tyson.
Sonia mtoto wa marehemu na Monalisa aliyekuwa mke wa marehemu Monalisa (kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Meck Sadick akizungumza kwenye msiba wa marehemu George Tyson
Mboni Masimba
Wasanii wa filamu Tanzania
Mchungaji akiongoza misa
Waombolezaji
Wafanyakazi wa TV 1 alipokuwa akifanya kazi marehemu mara ya mwisho kabla ya umauti wakiaga
.Mboni Masimba Mtangazaji wa The Mboni Show akiwasili katika viwanja vya
Leaders club kwa ajili kuaga mwili wa marehemu George Tyson
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akiaga mwili wa marehemu George Tyson.
Sunday, June 1, 2014
Mwanamke Aliyebadili Dini Apata Utetezi
Afisa mmoja mwandamizi katika wizara ya maswala ya
kigeni nchini Sudan amesema kuwa mwanamke aliyepewa hukumu ya kifo kwa
kubadili dini yake ya kiislamu,Meriam Ibrahim atawachiliwa huru katika
kipindi cha siku chache zijazo.
Kumekuwa na shutma za kimataifa kuhusu hukumu aliyopewa mwanamke huyo.
Meriam Ibrahim anazuiliwa katika jela moja ambapo alijifungua mtoto wa kike juma hili.
Ameolewa na mkristo na pia amehukumiwa kuchapwa viboko mia moja kwa kuzini kwa sababu mwanamke wa kiislamu kuolewa na mkristo ni haramu kulingana na sheria za Sudan.
(By BBC)
Polisi wafyatua mabomu ya kutoa machozi Uturuki
Polisi nchini Uturuki wamefyatua mabomu ya kutoa machozi
jana Jumamosi(31.05.2014)wakiwatawanya waandamanaji katikati ya mji wa Istanbul
wakati wa kumbukumbu ya mwaka mmoja ya maandamano makubwa kuipinga serikali.
Polisi walijiweka katika mstari mrefu kuwazuwia wanaharakati ambao walitarajia kusoma taarifa yao katika uwanja wa Taksim na kuweka maua katika uwanja huo katika kumbukumbu ya vifo vya kiasi watu sita katika maandamano dhidi ya utawala wa waziri mkuu Tayyip Erdogan.
Watu wengine sita wameuwawa katika machafuko yaliyotokea bila kutarajiwa katika miezi iliyofuatia wakati hasira dhidi ya Erdogan na chama chake cha AK zikitokota.
Maandamano ya mitaani huenda ni kitu kitakachojitokeza mara kwa mara katika wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa rais hapo Agosti ambapo Erdogan anatarajiwa kugombea, lakini wachache wanatarajia hali hiyo kuzusha athari kubwa za kisiasa kwa kiongozi huyo ambaye ameshika wadhifa wa waziri mkuu mara tatu.
Afisa wa ngazi ya juu wa chama cha AK amesema siku ya Jumamosi kuwa Erdogan atagombea wadhifa wa urais na kuiongoza Uturuki hadi 2023.
Karibu na uwanja wa Taksim, mamia ya watu waliimba , "jiuzulu, wauwaji AKP" na "kila mahali ni Taksim, kila mahali ni upinzani" kabla ya polisi kufyatua gesi ya kutoa machozi dhidi ya kundi la watu, na kuwalazimisha kurudi nyuma
Subscribe to:
Posts (Atom)