Klabu inayoongoza ligi ya Uhispania almaarufu kama La Liga ATletico Madrid
usiku huu imefanikiwa kuingia fainali ya Klabu bingwa ya
Ulaya UEFA baada ya kuicharaza Chelsea ya Uingereza pale nyumbani kwake
darajani mbele ya mashabiki wake 3 - 1, ambapo sasa Atletico Madrid atakutana na
Real Madrid katika fainali timu zote
zikiwa ni kutoka nchini Hispania. Chelsea walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia
mchezaji wake Torres katika dakika ya 36 na dakika 44 kabla ya kupulizwa
filimbi ya mapumziko Atletico Madrid kupitia Adrian Lopez walisawazisha. Katika
dakika ya 60 Diego Costa aliipatia Atletico goli la pili kwa mkwaju wa penati
iliyosababishwa na Etoo baada ya kumsukuma kwa nyuma mchezaji wa Atletico
Madrid na goli lililokata matumaini ya Chelsea ni goli lililofungwa na Arda
Turan katika dakika ya 72. Katika mechi ya awali timu hizo zilitoka 0 – 0.
Atletico Madrid kwa mara ya kwanza inafika fainali ya Klabu bingwa ya Ulaya baada ya
miaka 40.
No comments:
Post a Comment