Shirika la Kazi
Ulimwenguni ILO limebainisha kwamba kazi za ndani zinazofanywa na wasichana
walio chini ya miaka 18 katika mazingira ya kitumwa, hatari au kinyonyaji ni
aina ya utumikishwaji wa watoto unaotakiwa kutokomezwa kama ilivyoainishwa
kwenye mikataba ya kimataifa.
Mikataba
hiyo inapinga utumikishwaji huo kufuatia kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa
kijinsia, udhalilishaji, kunyimwa chakula, kubakwa na kulipwa mishahara kiduchu
huku wahusika wakishindwa kuripoti kwa wazazi au katika vyombo vya usalama.
Umaskini
umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kwenda
kutumikishwa majumbani, hata hivyo sababu ya ukosefu wa elimu inawagusa baadhi
ya wazazi nchini
Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu LHRC ni moja ya taasisi zilizo mstari wa mbele
katika kutetea haki za wasichana wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na waajiri
wao.
Wachungaji
ni moja ya kundi linalowajibika kwa kiasi kikubwa kuhakikisha jamii haiendi
kinyume cha mila, desturi na maadili ya Kitanzania, Mchungaji FESTUS SAMBWE wa
Kanisa la Tanzania Assembles Of God Kihonda Morogoro ametoa wito kwa
wazazi kujiepusha na tabia kuwaruhusu watoto kujiingiza kwenye ajira zisizo
rasmi.
Tayari
tumeshuhudia athari, madhira na changamoto wanazokumbana nazo wafanyakazi wa
ndani ambao wazazi wamewafanya kama miradi katika kuwakomboa kwenye umaskini.
No comments:
Post a Comment