Jamii
imehimizwa kuwa karibu na jeshi la polisi katika kuhakikisha hakuna
wahalifu wanaojipenyeza katika mitaa na kusababisha uharibifu wa amani pamoja
na mali za wananchi.
Akiongea
katika uwekaji wa jiwe la msingi la kituo kikubwa cha polisi kinachotarajiwa
kujengwa katika kata ya Segerea jijini Dar es salaam ,Naibu mkuu wa jeshi la
polisi nchini ABRAHMANI KANIKI, amesema kuwepo kwa kutuo hicho
kutasaidia sana kuondoa wasiwasi wa raia na mali zao.
Wakiongea katika
uzinduzi huo Mbunge wa jimbo hilo ambae pia ni Naibu waziri wa kazi
na ajira MAKONGORO MAHANGA na diwani wa kata hiyo AZURI MWAMBIJI wamesema
katika kutumikia jamii wameweka tofauti zao pembeni ili kuhakikisha wananchi wa
eneo hilo wanapata kituo kikubwa cha polisi kwa ajili ya kuimarisha
usalama.
Katika
uzinduzi huo uongozi wa Bank ya posta TANZANIA umekabidhi hundi ya shilingi
million kumi kama mchango wao kwa ujenzi wa kituo hicho.
No comments:
Post a Comment