Shirika la
kutetea wanawake nchini Nigeria limeitisha maandamano ya wanawake milioni moja
katika mji mkuu , Abuja kupinga kushindwa kwa serikali kuwaokoa mamia ya
wasichana wa shule waliotekwa nyara na Boko Haram.
Wazazi
waliojawa ghadhabu wameishutumu serikali ya Nigeria kwa kushindwa kuwaokoa
wasichana hao waliotekwa nyara kutoka shule moja ya upili katika mji wa Chibok
lililopo jimbo la Borno tarehe 14 mwezi huu.
Shambulizi
hilo linaloshukiwa kufanywa na waasi wa Boko Haram ni miongoni mwa mabaya zaidi
kuwahi kuripotiwa nchini humo katika kipindi cha hivi karibuni yanayolenga
asasi za elimu.
Ghadhabu
nchini humo zimeongezeka zaidi kutokana na jeshi la nchi hiyo kushindwa
kuwapata wasichana hao zaidi ya wiki mbili sasa.
Maafisa wa
jimbo la Borno wamesema kiasi cha wanafunzi 129 walitekwa nyara na wapiganaji
wa Boko Haram waliowalizimisha kuingia katika msafara wa malori na kutorokea
msituni na 52 kati ya wasichana hao waliweza kujiokoa.
No comments:
Post a Comment